Sunday, June 17, 2012

TUTACHEZA KWA HESHIMA YA MASHABIKI WETU.

MSHAMBULIAJI wa timu ya Ireland ambaye pia ndiye nahodha wa kikosi hicho, Robbie Keane amesema kwamba nchi yake hiyo itacheza mchezo wa mwisho kwa ajili ya heshima lakini hawana walichokibakiza katika michuano. Ireland ambayo inanolewa na kocha Cesare Prandelli imepoteza michezo yake yote miwili ambapo katika mchezo wa kwanza walifungwa na Croatia mabao 3-1 na mchezo uliofuata walifungwa na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Hispania kwa mabao 4-0 hivyo kuiacha timu hiyo ikiwa haina alama yoyote katika kundi C. Lakini nchi hiyo ikiwa ni mojawapo ya nchi ambazo zimesafiri na mashabiki wengi zaidi, Kean anasisitiza kuwa ni muhimu timu hiyo kushinda mchezo wa kesho ili angalau waweze kuondoka na pointi katika michuano hiyo. Keane ambaye anacheza katika klabu ya Los Angeles Galaxy ya nchini Marekani ameendelea kusema kuwa ni muhimu kupata alama katika mchezo huo ili kuwapoza mashabiki wao ambao wamesafiri kutoka mbali kushuhudia timu yao.

No comments:

Post a Comment