Sunday, June 17, 2012

IOC YAANI UCHUNGUZI KUHUSIANA NA UCHAKACHUAJI WA TIKETI.

KAMATI ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC imeanza uchunguzi kuhusiana na tuhuma wawakilishi wa michuano hiyo mwaka huu kuwa na mpango wa kulangua maelfu ya tiketi za michuano hiyo itakayofanyika jijini London. Bodi ya maofisa wa IOC imekutana kufuatia tuhuma zilizotolewa na gazeti la kila siku la Sunday Times ambapo lililotoa taarifa kwamba nchi zaidi ya 50 zinahusika na mpango huo wa kulangua tiketi. Katika taarifa yake gazeti hilo lilisema kuwa tiketi kwa ajili ya michezo mikubwa zinatarajiwa kupatikana zikiwa na thamani iliyopanda mara 10 zaidi ya bei yake halisi. Waandaaji ya michuano hiyo walipinga tuhuma hizo pamoja na kwamba gazeti hilo lilitoa na vithibitisho kwamba maofisa wa Olimpiki pamoja na mawakala walikutwa wakiuza tiketi hizo kwa kulangua. Katika uchunguzi wake IOC pia litaangalia upya suala la usambazaji wa tiketi kwa nchi wanachama wa Olimpiki ambapo zaidi ya tiketi milioni moja zilisambazwa kwa nchi ambazo zitashiriki michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment