Saturday, June 9, 2012

TANZANIA POLITICAL NEWS: BOB MAKANI AFARIKI DUNIA


Kiongozi wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na muasisi wa chama hicho, na wakili wa siku nyingi, Bob Makani amefariki dunia jijini Dar es Salaam. habari zaidi kuhusu kifo hicho hazijapatikana.

Lakini taarifa zilizopatikana kwenye mitandao ya kijamii usiku wa kuamkia leo zimesema kwamba Bob amefariki baada ya kuugua kwa muda sasa.

Itakumbwa kwamba mwezi Mei mwaka huu Bob Makani akiwa Mbezi Jijini Dar es Salaam ali thibitisha kuwa kwa muda wa miaka mitatu sasa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiungulia na kizunguzungu kiasi cha kushindwa kwenda kazini. 

No comments:

Post a Comment