Saturday, June 9, 2012

TANZANIA SOCIAL NEWS: WAASWA KUCHANA NA WALIMU WA KIGENI

WAMILIKI wa shule binafsi wametakiwa kuacha kutoa ajira zaidi kwa walimu wa mataifa ya nje na badala yake wachukue walimu wa kitanzania ambao wanauwezo ili kuepusha shule zao na udanganyifu wa mithiani

Kauli hiyo imetolea mjini Arusha na Afisa elimu wa manispaa ya Arusha Bw. Omary Mkombole wakati akiongea na wanachama wa Tamongsco ambao ni wamiliki pamoja namameneja wa shule mbalimbali jiji humo.

Bw. Mkombloe alisema kuwa wamiliki hao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajiamini katika kazi zao ili waweze kufikia malengo mbalimbali ambayo wanayatka lakini kama wataendelea  kuwathamini zadii walimu wa mataifa ya nje basi hawataweza kufikia malengo

Alisema kuwa kuongeza kingereza kwa mwalimu isiwe ni tija mojawapo ya kusababisha asilimia kubwa ya watu kuweza kuajiriwa bali wanatakiwa kuangalia sifa na vigezo vya mwalimu bora

Wakati huo huo mkaguzi wa elimu kanda ya kaskazini magharibi bw Victor Bwindiki aliwaambia walimu hao kuwa wanatakiwa kuwa wabiunifu dhidi ya shule zao za binafsi ili wali mu wasiwakambie ovyo

No comments:

Post a Comment