Saturday, June 9, 2012

MBEYA UPDATE: WAKUTWA NA BHANGI GRAMU 15, WALALA MAHABUSU


Jeshi la Polisi mkoani Mbeya  linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukutwa na bangi gramu 15, tukio lililotokea Juni 7 mwaka huu majira ya saa 12:55 jioni eneo la Machinjioni,Wilaya ya Rungwe.

Kamanda Diwani amewataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Damas David(31) na Lusekelo Mwakalomba,ambapo hujihusisha na uuzaji na matumizi ya bangi hizo na wote wapo mahabusu.

Aidha majira ya saa 10:45 jioni siku hiyo hiyo maeneo ya Katumba wilayani humo; Polisi walimkamata Bi.Sophia Luvanda(40) pamoja na wenzake 14 wakiwa na pombe ya moshi(Gongo) lita 4 na mtambo mmoja wa kutengeneza pombe hiyo.

Watuhumiwa ni wauzaji na wanywaji wa pombe haramu ya Gongo na mpaka sasa wote wapo mahabusu wakati upelelezi ukiendelea kuhusiana na tukio hilo na mara baada ya upelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayowakabili.

No comments:

Post a Comment