Wednesday, June 27, 2012

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

TFF.

POLISI MORO YAACHA 17, TZ PRISONS 11  
Klabu tano za Ligi Kuu ya Tanzania zimewasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) majina ya wachezaji ambao zimewakatishia mikataba/mikataba yao kumalizika au kuwaacha kwa ajili ya usajili wa wachezaji msimu wa 2012/2013. Kwa mujibu wa klabu hizo, Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha wachezaji 17 wakati Tanzania Prisons ambayo pia imepata hadhi ya Ligi Msimu huu imeacha wachezaji 11. Azam imekatisha mikataba ya wachezaji watatu. Wachezaji 12 wamemaliza mikataba yao katika klabu ya Kagera Sugar wakati wakati kwa upande wa Simba wachezaji waliomaliza mikataba ni wanne huku ikionesha nia ya kuwatoa kwa mkopo wengine wanne. Uhamisho wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu. Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu. Wachezaji walioachwa Polisi Morogoro ni Abdul Ibadi, Ally Moshi, Benedict Kitangita, Hassan Kodo, Hussein Lutaweangu, Hussein Sheikh, Juma Maboga, Mafwimbo Lutty, Makungu Slim, Mbaraka Masenga, Method Andrew, Moses Mtitu, Ramadhan Kilumbanga, Ramadhan Toyoyo, Said Kawambwa, Salum Juma na Thobias John. Tanzania Prisons imewaacha Adam Mtumwa, Dickson Oswald, Exavery Mapunda, Ismail Selemani, Lwitiko Joseph, Mbega Daffa, Mwamba Mkumbwa, Musa Kidodo, Rajab Ally, Richard Mwakalinga na Sweetbert Ajiro. Wachezaji waliomaliza mikataba yao kwa mujibu wa Kagera Sugar ni Cassian Ponera, Hamis Msafiri, Hussein Swedi, Ibrahim Mamba, Martin Muganyizi, Mike Katende, Moses Musome, Msafiri Davo, Said Ahmed, Said Dilunga, Steven Mazanda na Yona Ndabila. Azam imewasitishia mikataba wachezaji Tumba Swedi, Mau Bofu na Sino Augustino. Wachezaji waliomaliza mikataba Simba kwa mujibu wa klabu hiyo ni Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais Kago, Juma Jabu wakati Salum Kanoni mkataba wake unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka huu. Wachezaji ambao Simba inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Rajab Isihaka, Salum Machaku, Haruna Shamte na Shija Mkina.

DODOMA YAITAMBIA MBEYA COPA COCA-COLA 2012 Dodoma imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Juni 27 mwaka huu) kuifunga Mbeya mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko Kibaha mkoani Pwani. Mabao ya Dodoma katika mechi hiyo ya kundi C yalifungwa na Japhet Lunyungu dakika ya 59 wakati Frank Kaji aliwahakikishia ushindi washindi dakika saba kabla ya filimbi ya mwisho baada ya kupachika bao la pili. Nayo Mjini Magharibi iliifunga Iringa mabao 3-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani. Mechi za asubuhi zilizokuwa zichezwe leo kati ya Arusha na Kusini Pemba kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers na Pwani na Tabora kwenye Uwanja wa Karume sasa zitachezwa kuanzia saa 8 mchana kutokana na kutokuwepo mawasiliano ya barabara asubuhi (Morogoro Road) kutoka mkoani Pwani kuingia Dar es Salaam. Leo jioni kutakuwa na mechi kati ya Rukwa na Ruvuma (Tanganyika Packers), Mwanza na Tanga (Nyumbu), Kaskazini Unguja na Mara (Tamco) na Singida na Kagera (Karume).

No comments:

Post a Comment