Wednesday, June 27, 2012

ARSENAL KUJIPIMA NGUVU NA SUPER EAGLES JIJINI ABUJA.KLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza inatarajiwa kucheza kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Nigeria-Super Eagles kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi hiyo mchezo utakaopigwa jijini Abuja, Agosti 5 mwaka huu. Nigeria ambayo inashika nafasi ya 60 katika orodha za Shirikisho la Soka Duniani-FIFA itakutana na Arsenal ambayo ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza. Mratibu wa mchezo huo David Omigie alitangaza uwepo wa mchezo huo baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano ambapo Shirikisho la Soka la Nigeria-NFF limemuagiza kocha wa Super Eagles kuandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo. Kwa kawaida klabu ya Arsenal huwa inakuwa na mashindano ya kombe la Emirates katika kipindi hiki cha maandalizi lakini mwaka huu michuano hiyo haitafanyika kutokana na uwepo wa michezo olimpiki ambayo itafanyika jijini London. Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kutua katika ardhi ya Afrika toka mwaka 1993 wakati walipofanya ziara nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment