Thursday, June 21, 2012

TAARIFA KUTOKA TFF LEO.

MKUTANO MKUU WA DHARURA TWFA JUNI 23
Mkutano Mkuu wa Dharura wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utafanyika Juni 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre, Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa TWFA, Lina Kessy, ajenda kuu katika mkutano huo ni marekebisho ya Katiba ya chama hicho yanayotokana na maelekezo ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya marekebisho kwenye katiba za wanachama wake ambazo zina upungufu. Tayari mapendekezo ya marekebisho hayo kulingana na mwongozo wa TFF yalishapitiwa na Kamati ya Utendaji ya TWFA. Mbali ya Kamati ya Utendaji, wajumbe wengine wa mkutano huo ni Mwenyekiti, Katibu na mjumbe wa Mkutano Mkuu kutokana vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara. Wajumbe watafikia kwenye hosteli ya Msimbazi Centre ambapo wanatakiwa kuripoti siku moja kabla ya mkutano huo. Mgeni rasmi atakayefungua mkutano huo anatarajiwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda.

No comments:

Post a Comment