Thursday, June 21, 2012

TANZANIA POLITICAL NEWS: MAKINDA AWATAKA WABUNGE KUACHA VIJEMBE BALI WAJADILI BAJETI


SPIKA wa Bunge Anne Makinda amewataka wabunge warudishe heshima ya Bunge kwa kuacha tabia za kupigana vijembe wakati wanapochangia Bajeti ya Serikali.

Makinda amesema michango ya wabunge ni muhimu katika kuboresha Bajeti ya Serikali, hivyo kama wakiacha kuchangia na kuingia kwenye malumbano ya kisiasa, hawawezi kuisaidia Serikali na wananchi waliowatuma. Makinda ametoa mwito huo jana baada ya kipindi cha maswali na majibu baada ya siku mbili za mjadala wa bajeti hiyo kutawaliwa na malumbano ya kisiasa hali iliyowalazimisha wabunge kutoa lugha za kuudhi. Spika huyo alisema amepokea simu nyingi zinazowashutumu wabunge kuhusu hali iliyojitokeza katika mjadala wa bajeti kuanzia Jumatatu. Amesema wabunge wakiendelea kuonesha ubingwa wao wa kupiga siasa katika kujadili bajeti hiyo, wananchi waliowatuma watasikitishwa na hali hiyo. Amesema ushauri wa wabunge ni muhimu ili Serikali ijue iboreshe wapi na ipunguze wapi matumizi ili wananchi wapatiwe bajeti nzuri. Kiongozi huyo pia aliwaka wabunge hao wajihurumie wenyewe kwa mambo ya ajabu wanayofanya ukumbini ya kuonesha ubingwa wa kupiga siasa. Akiahirisha Bunge baada kumalizika kwa kipindi cha asubuhi, Spika Makinda alieleza kuridhishwa na michango ya wabunge waliochangia kuanzia asubuhi.

Kutokana na mabadiliko hayo, Makinda alisema sasa mjadala wa bajeti utakuwa wa siku tano badala ya nne na hivyo utahitimishwa kesho Ijumaa.

No comments:

Post a Comment