Thursday, June 21, 2012

MBEYA UPDATE: RC KANDORO AWATAKA WAKAZI WA MOMBA KUWA NA USHIRIKIANO


Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka viongozi na wananchi wa wilaya Mpya ya Momba kuhakikisha wanakuwa na mshikamano ili kuiwezesha wilaya yao kupata maendeleo kwa haraka.

Kandoro ameyasema hayo katika sherehe za kuipongeza serikali kwa kukubali ombi la kuanzishwa kwa wilaya ya Momba zilizoandaliwa na wananchi na kufanyika katika kijiji cha Chitete yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.

Amesema migongano na vitendo vya uvunjifu wa amani vinaweza kusababisha wilaya yao kuchelewa kuyafikia maendeleo hatua ambayo itakuwa inatofautiana na malengo ya serikali ya kuchukua maamuzi kuanzisha wilaya mpya.

Amewataka maofisa na watendaji wa serikali wilayani hapo kuhakikisha wanazingatia uadirifu katika utendaji kazi wao wakiogopa uonevu lakini pia wakizingatia kutokuwa waoga.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Abiud Saidea ameahidi kushirikiana kwa karibu na watendaji pamoja na wananchi huku pia akiiomba serikali ya mkoa kuhakikisha inakuwa karibu na kuipa upendeleo wilaya yake katika mipango mbalimbali ya kimaendeleo iliyopo.

Imeandikwa na Joseph Mwaisango, Mbeya

No comments:

Post a Comment