Thursday, June 21, 2012

SI KWELI HISPANIA HAWANA KIWANGO - LOEW.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amesisitiza kuwa Hispania bado wana nafasi kubwa ya kutetea uningwa wao wa michuano ya Ulaya wakati Ujerumani ikijiandaa kupambana na Ugiriki katika mchezo war obo fainali kesho. Ujerumani ambao wlifungwa na Hispania katika fainali ya michuano hiyo mwaka 2008, ndio timu pekee katika michuano hiyo ambayo imeweka rekodi ya kushinda mihezo yake yote mitatu katika kundi B. Hispania ambao walikuwa katika kundi C walishinda mabao 4-0 dhidi ya Ireland katika mchezo wa kwanza na baadaye kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Italia kabla ya kupanda ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Croatia Jumatatu. Kikosi cha Hispania ambacho kinanolewa na Vicente del Bosque Jumamosi kitakwaana na Ufaransa jijini Kiev, wakati Ujerumani itacheza na Ugiriki kesho lakini Loew amesema kuwa hawezi kubweteka na habari kuwa Hispania wanacheza chini ya kiwango katika michuano michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment