Thursday, June 21, 2012

SHABIKI WA IRELAND AKUTWA AMEKUFA KATIKA MFEREJI NCHINI POLAND.

Picha ndogo ni marehemu James Nolan na picha ni polisi wakihangaika kuokoa mwili wake uliokuwa katika mfereji.
MAOFISA wa polisi nchini Poland wamesema kuwa mwili uliokutwa ukielea katika mfereji umegundulika kuwa ni wa mshabiki soka wa Ireland ambaye alikuwepo nchini humo kwa ajili ya michuano ya Ulaya. Mwendesha mashitaka msaidizi nchini humo, Wlodzimierz Marszalkowski aliviambia vyombo vya habari Jumatano kuwa mmoja wa mtu aliyedai kuwa karibu na familia hiyo ya kijana huyo alithibitisha kuwa ni mwili wa James Nolan ambaye alipotea mapema Jumapili katika mji uliopo Kaskazini mwa nchi hiyo wa Bydgoszcz. Nolan ambaye ana umri wa miaka 21 alipotea Jumapili katika mji huo ambapo juhudi za kumtafuta zilizaa matunda jana baada ya polisi wa kikosi cha uzamiaji walipoupata mwili huo jana na wanasubiri wazazi wa kijana huyo kuja kutambua kama ni kijana wao. Mwendesha mashitaka huyo amesema kuwa hakuna dalili za kuporwa kwa kijana huyo baada ya kukutwa na kiasi cha dola 200 pamoja na kadi zake za benki katika maiti yake ambapo wanatarajia kuufanyia uchunguzi mwili huo ilikujua kiini haswa cha kifo chake.

No comments:

Post a Comment