Wednesday, June 20, 2012

SHEVCHENKO ATUNDIKA DALUGA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ukraine, Andriy Shevchenko ametangaza kustaafu soka la kimataifa kufuatia nchi yake kuondolewa katika hatua ya makundi ya michuano ya Ulaya. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 aliingia akitokea benchi la wachezaji wa akiba ukiwa ni mchezo wake wa 111 akiwa na kikosi cha nchi hiyo ambapo walikubali kipigo cha bao 1-0 na Uingereza. Shevchenko alikuwa nahodha wa nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 ambapo kikosi hicho kilitolewa katika hatua ya robo fainali na pia aliwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2004. Mchezaji huyo ameitumikia timu yake ya taifa kwa zaidi ya miaka kumi akiwa ameweka rekodi ya kufunga mabao 48 ambapo bao lake la kwanza kufunga ilikuwa ni mwaka 1996 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Uturuki na mabao mawili ya mwisho alifunga dhidi ya Sweden katika michuano ya Ulaya mwaka huu. Shevchenko amewahi kushinda kombe la Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2003 akiwa na AC Milan kabla ya kuhamia Chelsea mwaka 2006 ambapo hakupata mafanikio sana kama ilivyokuwa kwa Milan. Kwasasa mchezaji huyo anacheza katika klabu ya Dynamo Kiev na mkataba wake unatarajiwa kuisha mwezi ujao ambapo kuna tetesi kuwa atahamia katika Ligi Kuu nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment