Wednesday, June 20, 2012

AL AIN YATHIBITISHA KUMNYAKUWA GYAN MOJA KWA MOJA.

OFISA Mkuu wa klabu ya Al Ain ya Falme za Kiarabu-UAE, Carlo Nohra amesema kuwa mkataba wa kudumu wa mshambuliaji nyota kutoka Ghana Asamoah Gyan umeshakamilika kwa asilimia 95. Gyan ambaye ana umri wa miaka 26 msimu uliopita alicheza Al Ain kwa mkopo akitokea klabu ya Sunderland na kufunga mabao 22 ambayo yaliiwezesha klabu hiyo kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu ya UAE. Mshambuliaji huyo alijiunga na klabu hiyo kwa ada ya euro milioni sita na kama klabu hiyo ikiamua kumyakuwa moja kwa moja itatakiwa kuongeza kiasi cha euro milioni tatu na nusu. Nohra amesema kuwa hawajatoa taarifa rasmi kwasababu kuna baadhi ya mambo bado hayajakamilika lakini karibu asilimia 95 imeshakamilika hivyo wanategemea mapema mwezi ujao kutangaza rasmi kumyakuwa mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment