Monday, June 25, 2012

MBEYA UPDATE: WATUHUMIWA 89 WAKAMATWA KATIKA SIKU 17


W
atuhumiwa 89 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo makosa 1895  ya usalama barabarani.

Akizungumza na waandishi habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Diwani Athumani amesema watuhumiwa 89 wamekamatwa na hadi hivi sasa 71 wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.

Kamanda Athumani amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika kipindi cha siku 17 tangu Juni 8 hadi Juni 25 mwaka huu huku wengi wakipatikana na makosa ya kukutwa mtambo wa gongo mmoja na kukutwa na gongo Lita 85 ½ .
Pia amesema makosa akali ya 1895 ya barabarani yamekamatwa huku 1701 yakitozwa faini kutokana na makosa hayo.

Hata hivyo Kamanda Athumani amezitaka taasisi za dini mkoani hapa kuendelea kukemea maovu katika majengo ya ibada ili uhalifu katika mitaa ya mkoani Mbeya kuwa salama.

No comments:

Post a Comment