Wednesday, June 27, 2012

MBEYA UPDATE: WANAWAKE WANYANYASWA IFIGA

K
ushamiri kwa mfumo dume katika wilaya ya Mbeya kunaathiri kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi kwa wanawake ambao ndio nguvu kazi kubwa katika kilimo, kipato wanmachopata baada ya mavuno huishia mikononi mwa wanaume wanaojihusiusha na vitendo vya starehe na kusahau malezi ya familia zao.

Uchunguzi umebaini kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji na ukatili wanavyofanyiwa wanawake wa vijiji vya Ifiga,Iwalanje na Nsongwi juu  Kata ya Ijombe vinavyotokana na nguvu ya wanaume ya kuhodhi mali zilizopatikana kwa kuwashirikisha wanawake.

Mmoja wa wanawake wa Kijiji cha Ifiga Bi Salah Jailos alisema kuwa wakati wa  msimu wa kilimo unapowadia  hushirikiana na waume zao kwa karibu bila kuwepo ugomvi wowote ndani ya familia zao mpaka  mazao yanapokomaa.

Alisema kuwa inapofika kipindi cha kuvuna wanaume  huanza kubadilika kwa kutafuta sababu mbali mbali  za kuonyesha chuki ndani ya nyumba ili aweze kupata sababu za kuvuna peke yake mazao na kuuza pepe yake bila kumshirikisha mke wake.

Mwanamke mwingine mkazi wa Usongwe Juu Bi.Benadeta Hamisi alisema kufutia vitendo hivyo vya wanaume tunaomba waache kwani iweje wakati wa kilimo  tulime wote lakini inapofika wakati wa mavuno wawe wababe wa kuuza mazao9 peke yao kwa ujumla huu ni ukatili wa kijinsia kwa sisi wanawake wa Kata ya Ijombe.

Hata hivyo mwanamke huyo alisema athari ambazo wanapata baada ya kuachiwa familia ni kupata shida ya  kuhudumia familia ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto namahitaji mengine ya nyumbani ambayo ni muhimu.

Akizungumzia malalamiko hayo kwa Wanawake wa vijiji hivyo, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ifiga Bw.Raphael  Siyejele alisema hana taarifa za kiofisi za wanaume kuwanyanyasa wake zao labda kama zipo ngazi zingine.

No comments:

Post a Comment