Wednesday, June 27, 2012

MBEYA UPDATE: MABATINI WALALAMA UCHAFUZI WA KIWANDA CHA FAMILY LOAF


W
ANANCHI wa kata za Itiji na Mabatini katika  Halmashauri ya jiji la
Mbeya hivi karibu wamekitolea lawama kiwanda cha kuoka mikate cha Family Loaf kutokana na kitendo cha kiwanda hicho kutupa taka kwenye mto wa Mabatini ambao unatumiwa na wananchi hao.


Wananchi wa kata hizo, wamesema kiwanda hicho kimekuwa kikitupa
taka ndani ya mto huo ambao hutumika kwa shughuli za kibinadamu na
mifugo hata kusababisha wananchi kupata hofu kwa maelezo kuwa taka
hizo zinaweza kuwa na madhara kutokana na kemikali zilizomo ndani ya
taka hizo.

Angel Davis mkazi wa Itiji amesema kuwa ,mbali ya kuwepo hofu ya hizo
kemikali pia kitendo hicho ni cha uchafuzi mazingira na kukiuka haki
za binadamu na viumbe vingine vinavyo tumia maji ya mto huo.

Meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Omary Abdalah alipohojiwa na
amekiri kuwa eneo la Mabatini ni eneo ambalo limekuwa likitumiwa na kiwanda kuhifadhi taka baada ya watu wa jiji kushindwa kusomba taka mbali ya kutozwa ushuru 50,000 kwa mwezi wa idara ya  afya.

Hata hivyo amesema kwamba hana uhakika kama taka hizo zinatupwa ndani
ya mto kwa maelezo kuwa mtu anaye husika na utupaji taka aliagizwa
kutupa kwenye Guba la taka lililopo Mabatini wala si vinginevyo.

Hata hivyo,Meneja uzalishaji alipoulizwa kuhusu ubora wa bidhaa ya
kiwanda hicho alishindwa kutoa maelezo ya kina huku akisema mamlaka ya
chakula na dawa (TFDA) walifika kiwandani hapo kuchukua bidhaa
inayozalishwa hapokiwandani kwa uchunguzi lakini hadi leo hawajapatiwa
majibu lakini wakati huo mikate yake haina hata nembo ya TBS.

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Idd Jumanne alipoulizwa kuhusiana na
uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho ,alishindwa kukiona
kwenye mtao wa Kompyuta hivyo kueleza kwamba kiwanda hicho kinaendesha
shughuli kinyemela ambapo ni makosa kisheria.

Amesema kwamba,ili kubaini kinachoendelea kiwandani hapo aliahidi
kupeleka wataalamu wake wa mamlaka ya chakula na dawa huku akisisitiza
kuwa ana wasiwasi hata ushuru wa kusomba taka hatoi kwa maelezo kuwa
jiji hupenya kwa wadau wote wa taka na kama gari halifiki ni wajibu
wake kupiga simu ili kupatiwa huduma badala ya kuchafua mto.

No comments:

Post a Comment