Wednesday, June 27, 2012

MBEYA UPDATE: WANANCHI WAMTIMUA MWENYEKITI WA KIJIJI


W
ananchi wa kijiji cha Bumbiji kata ya Isange Mwakaleli wilayani Rungwe mkoani Mbeya wamejikuta wakimwondoa mwenyekiti wa kijiji hicho baada ya kujihusisha na ubatilifu wa mali za kijiji hicho.
Akizungumza na kituo hiki afisa mtendaji wa kijiji hicho Aswile Mwalukasya amesema wananchi hao wameamua kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na imani na kiongozi huyo kutokana na ufujaji wa fedha za kijiji kiasi cha shilingi laki tano.

Mwalukasya ameongeza kuwa mwenyekiti huyo anagubikwa na tuhuma za uharibifu wa mali ya kijiji kama simenti yenye thamani ya shilingi laki mbili pamoja nauuzaji wa miti ya kijiji hicho yenye thamani ya shilingi laki tatu ambayo ilikuwa itumike katika ujenzi wa nyumba za walimu kijijini hapo.

Wananchi wa kijiji hicho wamemtaka mwenyekiti huyo arejeshe fedha hizo ili ujenzi wa nyumba za walimu iweze kukamilika na kuondoa uhaba wa nyumba za walimu kijijini hapo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya isanga amethibitisha kutukia kwa tukio hilo na kuwasihi wananchi hao kuwa na subira kwani sheria itachukua mkondo wake.

Imeandikwa na Boco Nyambege, Mbeya

No comments:

Post a Comment