Tuesday, June 19, 2012

MBEYA UPDATE: WADAU WA SOKA WATAKIWA KUISAIDIA TIMU YA COPA COCA COLA

Ikiwa imebakia siku moja kwa Timu ya Soka kwa Vijana wa Kiume U 17 Copa Coca Cola mkoa wa Mbeya kuondomkoani humo kwenda Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya michuano hiyo itakayoanza kutimu vumbi hivi karibuni wito umetolewa kwa wananchi na wadau wa michezo mkoa humu kujitolea kwa hali na mali.

Kwa nyakati tofauti Kocha wa timu hiyo Maka Mwalwisi na Katibu wa MREFA Laurence Mwakitalu wamsema timu ya sasa ni nzuri kuliko maelezo kutokana na mwamko wa soka mkoani humo.Hivyo basi changamoto inayowakabili ni huduma za msingi kwani wanapenda kuona vijana hao wakisonga mbele katika kuendeleza vipaji vyao kwa kupata mahitaji muhimu wawapo katika michuano hiyo. 

Pia wamesema kucheza vizuri katika michuano hiyo kutawafanya waonekane katika Ulimwengu wa Soka wanapokuwa katika mazoezi wanatakiwa wasiwaze mambo mengi zaidi ya soka lakini hiyo itachangiwa na mahitaji muhimu kupatikana. Haya yanajiri kufuatia udhaminiwa Coca Cola kuwa kidogo msimu huu licha ya kwamba wanaamini wadau na wapenda soka watajitoa kwa hali na mali kwa vijana hao kuifanikisha safari yao ya kwenda na kurudi huku wakiwa bna Kombe la Michuano hiyo mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment