Tuesday, June 26, 2012

MBEYA UPDATE: MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA AGONGWA NA GARI AFA PAPO HAPO


M
wanafunzi wa Darasa la  Kwanza katika Shule ya Msingi Ilomba Edward Jackson (10) amekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari ambalo halikufahamika mara moja juzi majira ya saa 1:00 jioni maeneo ya Sae Jijini Mbeya.
Taarifa ya Jeshi la Polisi kwa Vyombo vya habari imesema ajali hiyo imetokea katika barabara ya Mbeya-Iringa na chanzo chake ikiwa ni mwendo kasi na dereva alikimbia mara baada ya tukio hilo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya na Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wasamaria wema kutoa taarifa zitakazoweza kusaidia kupatikana kwa mtuhumiwa ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa. Wakati huo huo Jeshi la polisi mkoani Mbeya limekamata gramu 624 za banghi katika kijiji cha Ichenjezya wilayani Mbozi juzi majira ya saa 6:00 mchana ambazo zilifichwa kwenye mfuko wa rambo kichakani. Maafisa wa Jeshi la Polisi wametaja majina ya watuhumiwa ni Naseeb Paul (30), Mnyakyusa na  mkulima pamoja na Waziri Chengwa (21), Mbena na mkulima wote wakiwa wakazi wa Ichenjezya.Pia Maafisa wa Polisi wamesema,  watuhumiwa hao ni wauzaji na watumiaji wa dawa hizo za kulevya ambayo yamepigwa marufuku hapa nchini Tanzania. Watuhumiwa wapo mahabusu wakisubiri hatua za kisheria ili wafikishe mahakamani. 

Hayo yanajiri ikiwa ni siku ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya .

No comments:

Post a Comment