Tuesday, June 26, 2012

KONA YA MWALIMU: DAWA ZA KULEVYA

DAWA ZA KULEVYA
Kwa mujibu wa Mwongozo wa kisasa wa Utambuzi na Takwimu ya Matatizo ya Akili (DSM-IV), utegemezi wa vileo unafafanuliwa kama:

"Wakati mtu anaposhikilia matumizi ya pombe au dawa nyinginezo licha ya matatizo yanayohusiana na matumizi ya kileo hicho, utegemezi wa kileo unaweza kuaguliwa.Matumizi ya kimazoea na ya kila mara huweza kusababisha uzoeaji athari za dawa na dalili za kuacha wakati matumizi yanapopunguzwa au kukomeshwa. Haya, pamoja na matumizi mabaya ya vileo hujumuishwa kama matatizo ya utumiaji bidhaa za kulevya ...." [1]

Utegemezi wa kileo unaweza kutambulliwa kwa utegemezi wa kimwili , ushahidi wa kuzoea au kuacha, au bila utegemezi wa kimwili.

Dhana yenye ukuruba ya utegemeaji wa dawa za kulevya ina fafanuzi nyingi tofauti. Baadhi ya waandishi kwa kweli hutoa maana sawa kwa dawa za kulevya na utegemeaji wa vileo, wengine kwa mfano hutoa ufafanuzi finyu kwa dawa za kulevya ambao hutenga dawa zisizo na ushahidi wa kuzoeleka au dalili za kuacha.

Istilahi matumizi mabaya na uzoelevu wa dawa za kulevya zimeweza kufafanuliwa na kufafanuliwa upya kwa miaka mingi. Kamati ya Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani ya 1957 Shirika la Afya Duniani(WHO) kuhusu dawa zinazosababisha utegemeaji wa kulevya walifafanua-utegemezi kwa vileo na uzoevu kama sehemu ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya:

Matumizi ya dawa za kulevya ni hali ya ulevi wa muda au wa kila mara unaotokana na matumizi ya mara kwa mara ya dawa (asili au sanisi). Sifa zake ni pamoja na: (i) utashi mkubwa au uhitaji (wa kimazoea) wa kuendelea kutumia dawa ya kulevya na kuitafuta kwa njia yoyote ile; (ii) tabia ya kuongeza kiwango, (iii) utegemeaji wa kiakili (kisaikolojia) na wa kimwili kwa jumla kwa athari za dawa za kulevya, na (iv) athiri mbaya kwa mtu binafsi na kwa jamii.

Uzoevu wa dawa (tabia) ni hali inayosababishwa na matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kulevya. Sifa zake ni pamoja na (i) utashi (lakini siyo ya kimazoea) wa kuendelea kutumia dawa za kulevya kwa minajili ya kuhisi ustawi wa kihali ambayo huibushwa; (ii) tabia ya kuongeza kiwango kidogo au kutoongeza , (iii) kiasi fulani cha utegemeaji wa kiakili kwa athari za dawa za kulevya, lakini bila ya utegemezi wa kimwili na hivyo ni wa dalili za kuacha [kujiondoa], na (iv) madhara mabaya, iwapo yapo, hasa kwa mtu binafsi.
Katika mwaka wa 1964, kamati mpya ya WHO iligundua kuwa fafanuzi hizi ni duni, na kupendekeza matumizi ya istilahi ya kijumla ya "utegemezi wa dawa za kulevya":

Ufafanuzi wa neno kulevya ulipata ukubalifu, lakini utata katika matumizi ya istilahi matumizi ya dawa za kulevya na uzoevu na matumizi mabaya uliendelea. Aidha, orodha ya dawa za zilizotumika vibaya iliongezeka kiidadi na kwa wingi. Utata huu umezidi kubainika wazi na jitihada mbalimbali zimefanywa kutafuta istilahi inayoweza kutumika kwa ujumla kuelezea matumizi mabaya ya dawa za kulevya . Dhana ya kimsingi katika yote mawili inaonekana kuwa utegemezi, ama wa kiakili au wa kimwili . Kwa hivyo, matumizi ya neno 'utegemezi wa dawa , yanayojumuisha awamu ya kimpito huihusisha na aina mahususi ya dawa ili kutofautisha aina moja ya dawa ya kulevya na nyingine, yalipewa uzingativu wa makini sana. Kamati ya wataalamu inapendekeza matumizi ya neno 'utegemeaji wa dawa' badala ya 'matumizi ya dawa za kulevya' na 'uzoevu wa dawa za kulevya'.

Kamati hiyo haikufafanua kikamilifu utegemezi, bali aliendelea mbele na kubainisha kuwa palikuwa na tofauti kati ya utegemezi wa kimwili na kisaikolojia ("kiakili"). Ilieleza kuwa matumizi mabaya ya dawa za kulevya ilikuwa"hali ya utegemezi wa kiakili au utegemezi wa kimwili, au yote mawili, kwa dawa za kulevya, ambayo hudhihirika kwa mtu kufuatana na matumizi ya dawa hiyo kwa vipindi vifupi au vinavyodumu kwa muda." Utegemezi wa kiakili ulifafanuliwa kama hali ambapo "pana hisia za kuridhika na msisimko wa kiakili ambao huhitaji matumizi ya dawa ili kuibusha raha au kuepusha usumbufu" kwa muda mfupi au muda mrefu " na dawa zote za kulevya zilisemekana kuwa na uwezo wa kuibusha hali hii:

Ni nadra sana kupata hali ambapo kitu chochote kinachoingizwa mwilini kitashindwa kuwasababisha baadhi ya watu kuathirika kwa msisimko wa kuridhika au kufurahia, kwa namna inayowashawishi kuendeleza matumizi yake hadi kufikia kiwango cha matumizi mabaya - yaani, kutumia kupita kiasi au kutumia zaidi ya invyohitajika kimatibabu.

Mwaka 2001, Chuo cha Marekani cha Dawa za Maumivu , Shirika la Maumivu Marekani na Shirika la Marekani la Dawa za kulevya, kwa pamoja zilitoa "Fafanuzi Zilizohusiana na Matumizi ya Opioidi kwa kutibu maumivu"

No comments:

Post a Comment