Tuesday, June 26, 2012

AFRICA NEWS: MURSI AKUTANA NA BARAZA LA KIJESHI

Rais mteule wa Misri, Dkt. Mohammad Mursi amekutana na Baraza la Kijeshi la nchi hiyo kujadili mamlaka ya ofisi ya rais.
Habari zinasema kuwa rais huyo mteule pia amejadili suala la kuunda baraza la mawaziri litakalokuwa na sura ya kitaifa. Duru za karibu na mkutano huo zimesema kuwa, Dkt. Mursi amelalamikia hatua ya jeshi ya kuipokonya ofisi yake madaraka yote.
Huku hayo yakijiri, Ahmed Shafiq, Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa Hosni Mubarak ambaye alishika nafasi ya pili kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa rais ameelekea nchini Saudi Arabia baada ya vyombo vya sheria vya Misri kuanza uchunguzi wa tuhuma za ufisadi dhidi yake. Wapambe wa Shafiq wamedai kwamba mwanajeshi huyo wa zamani ameelekea Saudia kwa ajili ya ibada ya Umra lakini wachambuzi weledi wa mambo wanaamini kuwa Shafiq ametoroka kwa kuhofia kuwa huenda rais mpya akaamua kumuandama

1 comment:

  1. eToro is the #1 forex trading platform for newbie and pro traders.

    ReplyDelete