Friday, June 22, 2012

MBEYA UPDATE: MAMA WA MTANGAZAJI WA REDIO MBEYA FM APIGWA

Mama wa Mtangazaji wa Redio Mbeya FM, Stanslaus Lambert amepigwa vibaya na Kondakta wa basi la Abiria maeneo ya NaneNane Jijini Mbeya jana saa 1 jioni kufuatia kutoelewa yeye na kondakta huyo.

Katika mahojiano maalum na JAIZMELALEO mchana wa leo nyumbani kwake maeneo ya Isyesye mama wa Mtangazaji huyo amesema zogo lilianzia Soweto alipopanda basi baada ya Kondakta kumjibu vibaya kwa matusi mzee ambaye hakumfahamu jina ambaye ni sawa na babaye.

Baada ya hapo Mama huyo amesema alimwambia wewe ni mtot mdogo yaani Kondakta  kumjibu kwa matusi mzee huyo ndipo ugomvi ulipoanzia  kwani Kondakta alianza kumfurumishia matusi mkubwa ya nguoni.

Wakati anataka kushuka Kituo cha NaneNane  alipigwa ngumi kali ya uson uliyomfanya kuvuja damu, ndipo abiria walipochachamaa kumtaka dereva na kondakta wafikishwe polisi kujibu kwani iliopnekana Kondakta alitumia kitu chenye ncha kali.

Abiria na mama wa mtangazaji walifika kituo cha Polisi kidogo cha Uyole na walipewa PF 3  kwa ajili ya matibabu na Kondakta yu mahabusu kwa ajili ya kujibu.

Stanslaus Lambert Mtangazaji wa Redio MBEYA  FM amesema inasikitisha kuona makondakta wakiingia katika kashfa ya kupiga abiria na kuongeza kwamba Mbeya kumekuwa na tabia ya madereva kuwa “ DEIWAKA” wasio na shughuli na kulitaka Jeshi la Polisi kushughulikia makondakta.
 GETI LA NYUMBA YA MAMA STANS
 STANS AKIINGIA
 STANS AKIZAMA NDANI ZAIDI

 MAMA STANS AKIZUNGUMZA JAMBO KWA JIRANI 


 MAMA STANS AKIJIHISI MAUMIVU
 MAMA STANSA AKIZUNGUMZA JAMBO
MAMA NA MWANA WAKITABASAMU BAADA YA JAMBO MOJAWAPO KUZUNGUMZA KATIKA KISA HICHO CHA KUSIKITISHA

No comments:

Post a Comment