Thursday, June 14, 2012

MBEYA UPDATE: KESHO NI SIKU YA MTOTO WA AFRICA


H
apo kesho ni siku ya Mtoto wa Afrika Mkoani Mbeya maandamano hayo yanadhimishwa  huku yakikabiliwa na changamoto lukuki.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Child Support Tanzania  Noel Msuya Shawa amezitaja changamoto mbalimbali ikiwemo sintofahamu kwa jamii ya kutetea watoto wenye ulemavu kufuatia dhana kuwa mtoto mlemavu hawezi chochote; hali inayosababisha  watoto hao kutengwa.

Pia Noel Msuya ameongeza kusema katika shule za msingi na sekondari kumekuwa na ukosefu wa vifaa vya watoto wenye ulemavu hali inayosababisha kusoma katika mazingira magumu.

Juni 15 mwaka huu kutakuwa na maandamano ya hiari kuanzia kituo cha Stereo Kona ya Kihumbe hadi Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya yakilenga kutetea haki za watoto wenye ulemavu nchini Tanzania.

Siku hiyo itapambwa na michezo mbalimbali ikiwemo ya watoto walemavu yenye malengo ya kuonyesha uwezo wao katika kazi na kuondoa sintofahamu miongoni mwa jamii.

Kauli mbiu ya mwaka huu Haki za Watoto wenye Ulemavu, jukumu letu kuzilinda, kuheshimu na kuwatimizia.

No comments:

Post a Comment