Thursday, June 14, 2012

MBEYA UPDATE: BAJETI ISIYOTEKELEZEKA HAIFAI


Mkutano wa ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kituo cha Mbeya kilichowakusanya madiwani na viongozi wa chama  hicho kutoka mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mbeya na Rukwa.
Mkutano huo umemalizika jana jioni katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya  kwa madiwani kutakiwa kuwa karibu na wananchi ili kujua changamoto zao na kuzitatua.

Mjumbe wa Kamati kuu Lazaro Titus Masai ambayeni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu amesema madiwani wao wameeleza changamoto mbalimbali wanazikabiliana nazo ikiwa ni pamoja na mipango ya halmashauri zao  kutotekelezeka kwa wakati hivyo kuonekana kama wanawadanganya wananchi.

Kwa upande wao madiwani wa Chama hicho waliohudhuria Semina hiyo ya Siku  Mbili wameitaka Serikali ya Tanzani kupanga bajeti ambayo inatekeleza ili kuondoa usumbufu kwa madiwani wao  kwa manufaa ya wananchi. Miongoni mwa waliozungumza alikuwa Diwani wa Kata ya Majengo, Songea Mjini Mkoani Ruvuma.

Katika suala la dini na ukabila Lazaro amesema CHADEMA hakina ubaguzi wa kidini na kikabila kama ambavyo wengi wamekuwa wakifikiria  hususani wakati huu wanapoeleka kuchukua dola.

No comments:

Post a Comment