Wednesday, June 20, 2012

MBEYA UPDATE: AFISA MTENDAJI LAWAMANI KWA KUKWAPUA PESA ZA MAENDELEO


O
fisa mtendaji wa Kata ya Nsalaga Bwana Cyprian Matola anatuhumiwa kuwadanganya watia saini benki na kuchukua shilingi milioni 2 na laki 8 za ujenzi wa sekondari ya kata kinyume cha taratibu.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Kamati teule iliyoundwa kufuatilia ujenzi wa shule ya sekondari Uyole, Jelly Mwakipesile wakati akitoa taarifa ya kamati kwenye kikao cha Maendeleo cha kata hiyo. Kamati hiyo iliundwa kutokana na kuwepo kwa taarifa, juu ya utaratibu mzima ambao haukuwa sahihi wa utoaji wa fedha benki na kupelekea kukwama kwa kazi hiyo ya ujenzi wa shule ya sekondari Uyole wakati fedha za ujenzi zilikuwa zimetolewa.             Aidha amesema fedha iliyokuwa ikichukuliwa benki na Ofisa Mtendaji Matola, ilikuwa inatunzwa UWAMU Saccos katika akaunti ya mtu binafsi hali iliyomfanya m,tendaji huyo awe anaizalisha fedha hiyo ya serikali kwa manufaa yake.

Nao wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya kata hiyo, walimtaka mtendaji Matola arudishe fedha hizo zilizotumika kinyume na taratibu na pia taarifa ifikishwe kwa Mkurugenzi wa jiji la Mbeya.

Jitihada za kumtafuta Mkurugenzi wa jiji, Juma Idd kuzungumzia suala hilo zimeshindikana kutokana na simu zake za kiganjani kutopatikana sanjari na kuwa nje ya ofisi kikazi.
Imeandikwa na Gabriel Mbwile, Mbeya

No comments:

Post a Comment