Sunday, June 17, 2012

MARADONA KUENDELEA KUINOA AL WASL.KOCHA wa klabu ya Al Wasl, Diego Maradona ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo pamoja na kutolewa katika fainali ya Ligi ya mabingwa na kusababisha bodi ya klabu hiyo kujiuzulu na kuzusha mjadala juu ya mustakabali wa Maradona. Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mohammad Ahmad bin Fahad alipuuza taarifa hizo zilizozagaa na kudai kuwa kikao cha bodi kilichofanyika hakikuwa cha kuzungumzia hatma ya Maradona kuendelea kuifundisha klabu hiyo. Bin Fahad amesema kuwa Maradona bado ataendelea kuwa kocha wa klabu hiyo hakutakuwa na mabadiliko yoyote katika nafasi yake hiyo kwasasa. Bodi ya Al Wasl ilijiuzulu Alhamisi bila kutoa sababu zozote na ilikuwa ikiongozwa na Marwan bin Bayat ambaye ndio aliyesababisha maradona kutia saini ya kuinoa klabu hiyo kwa miaka miwili.

No comments:

Post a Comment