Sunday, June 17, 2012

THE CRANES YALAMBA BONUS DOLA 28,000 KWA KUITOA CONGO BRAZZAVILLE.


 

TIMU ya taifa ya Uganda maarufu kama The Cranes jana mchana wamekabidhiwa kiasi cha dola 28,000 kamazawadi baada ya kuigaragaza congo Brazzaville kwa mabao 4-0. Rais wa Shirikisho la Soka nchini Uganda-FUFA, Lawrence Mulindwa alikabidhi fedha hizo kwa nahodha wa kikosi hicho Andy Mwesigwa katika hafla ya chakula cha mchana jijini Kampala ambapo wanatarajiwa kugawana kiasi cha shs milioni 2.5 kila mchezaji katika wachezaji 18 wa timu hiyo. Mabao yaliyofungwa na Mwesigwa, Godfrey Walusimbi, Geoffrey Massa na Emmanuel Okwi yalitosha kuipa Uganda ushindi wa jumla ya mabao 5-3 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa na timu hiyo mabao 3-1. Uganda sasa inaingia katika mzunguko wa mwisho ambapo itapangwa na timu yoyote ambayo iko katika nafasi 15 bora katika orodha za Afrika ambapo kama wakifanikiwa kushinda basi watakuwa wamekata tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment