Sunday, June 17, 2012

TOTTENHAM YAMUWANIA VILLAS-BOAS.


 

KLABU ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza imefanya mazungumzo na mwakilishi wa kocha wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas ikiwa ni mikakati ya klabu hiyo ya kutafuta kocha mwingine. Uongozi wa Spurs ulifanya mawasiliano na wakala wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 34 kuangalia uwezekano kwa kumchukua na kama akikubali anaweza kufanyiwa usaili baadae wiki hii. Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy amerejea jijini London leo na anatarajiwa kusimamia suala hilo mwenyewe ambapo mbali na Villas-Boas pia kocha wa Ufaransa Laurent Blanc naye pia amehusishwa kutua klabuni hapo. Wakala wa Villas-Boas alikuwa jijini London mwishoni mwa wiki hii pamoja na kwamba Spurs walisisitiza kuwa hawatakuwa na haraka ya kusaka kocha mwingine hivi sasa.

No comments:

Post a Comment