Saturday, June 2, 2012

LUCA TONI AFIWA NA MWANAWE.

MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Italia, Luca Toni amepatwa na msiba mkubwa baada ya kufariki kwa mwanae kabla ya kuzaliwa. Toni ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Al Nasri ya Dubai na rafiki yake wa kike ambaye ni mwanamitindo walikuwa wakitegemea motto wao wa kwanza lakini kichanga hicho kilifariki wakati kikizaliwa. Katika taarifa yake mchezaji huyo ambaye aliongea kwa masikitiko makubwa amesema kuwa alitegemea siku hiyo ingekuwa ya furaha kwao lakini tofauti walivyofikiria imekuwa siku ya huzuni kubwa kwao kwani mototo wao amekufa bila hata kuona mwanga wa jua. Toni mwenye miaka 35 ambaye alikuwepo katika kikosi cha Italia kilichonyakuwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 alijiunga na Al Nasri januari mwaka huu baada ya kushindwa kufikia makubaliano na klabu ya Juventus.

No comments:

Post a Comment