Saturday, June 2, 2012

RONALDINHO KUONDOKA BRAZIL.

NAFASI ya kiungo wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Ronaldinho kuendelea kusakata kabumbu nchini humo imekuwa ndogo kufuatia kukatizwa kwa mkataba wake na klabu ya Flamengo. Siku baada ya mchezaji huyo kukatiza mkataba na klabu hiyo na kuishitaki kwa kutomlipa mshahara wake, viongozi kutoka klabu mbalimbali nchini humo wamesema hawana nia ya kumsajili mchezaji huyo. Nia haswa ya kushindwa kumsajili Ronaldinho inatokana na kiwango kibovu alichokionyesha toka atue nchini humo pamoja na tabia zisizo na kiuanamichezo ambazo amaekuwa akizionyesha akiwa nje uwanja. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo mchezo ambaye ana miaka 32 amesema kuwa kwasasa anahitaji muda wa kupumzika kucheza soka ili amuuguze mama yake lakini wakati atapokuwa tayari ataangalia klabu ya kucheza ambayo itakuwa ya nje ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment