Saturday, June 2, 2012

MADRID NAO KUELEKEA NCHINI MOROCCO.

IKIWA ni siku chake toka klabu ya Barcelona itangaze nia yake ya kufanya ziara nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi, mahasimu wao klabu ya Real Madrid na wamesema kuwa watakwenda katika nchini hiyo iliyopo Kaskazini mwa bara la Afrika kwa madhumuni kama hayo. Kwa mujibu wa gazeti moja nchini Hispania Real Madrid wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wapya wa Ligi Kuu nchini Morocco klabu ya Moghreb Tetouan mchezo ambao utachezwa Julai 24 ikiwa ni siku nne kabla ya mahasimu wao Barcelona hawajawasili nhini humo. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa mchezo huo wa kirafiki kati ya Moghreb Tetouan na Reala Madrid utachezwa katika Uwanja wa Tanger. Gazeti la El Mundo Deportivo la Hispania lilithibitisha kiasi ambacho Barcelona itapata katika ziara yake nchini humo kuwa kinafikia kiasi cha zaidi ya euro milioni moja.

No comments:

Post a Comment