Wednesday, June 20, 2012

HULK AITAMANI CHELSEA.

MSHAMBULIAJI wa kimatifa wa Brazil na klabu ya Porto ya nchini Ureno, Hulk ameisafishia njia Chelsea ya kumsajili baada ya kukiri kuwa angependa kuichezea klabu hiyo kama akitua Uingereza. Mchezaji huyo anatarajiwa kuondoka Porto katika kipindi hiki cha usajili cha majira ya kiangazi na amekuwa akitakiwa na vilabu vingi Ulaya ambapo zaidi kwasasa ni klabu ya Paris St Germain ya Ufaransa ambayo nayo imeonyesha nia ya kumnyakuwa. Kwa muda mrefu klabu ya Chelsea wamekuwa wakihusishwa kumtaka mchezaji huyo hususani msimu uliopita wakati aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Andre Villas Boas kujaribu kumleta mchezaji huyo kabla hajatimuliwa. Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich anamuona mchezaji huyo kama atafaa kuziba pengo la aliyekuwa mshambuliaji wa klabu hiyo Didier Drogba ambaye amekimbilia nchini China kwenye klabu ya Shanghai Shenghua.

No comments:

Post a Comment