Wednesday, June 20, 2012

CAMERON AIPA TANO UINGEREZA.

WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron ametania kuwa anaweza kuacha kuunga mkono suala la mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli baada ya timu ya taifa ya nchi hiyo kunufaika na makosa ya mwamuzi katika mchezo wa makundi wa michuano ya Ulaya dhidi ya Ukraine. Uingereza ilifanikiwa kuifunga Ukraine bao 1-0 katika mchezo wa jana na kufanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo lakini baada ya bao la kusawazisha la Ukraine katika dakika ya 62 kukataliwa kimakosa na mwamuzi aliyedhani mpira ulikuwa haujavuka mstari wa goli. Akiulizwa kuhusiana na mchezo huo katika mkutano na waandishi wa habari katika mkutano wa G20 nchini Mexico, Cameron aliwapongeza wachezaji wa kikosi cha Uingereza na kuamini kuwa kikosi hicho kitafika mbali kwenye michuano hiyo. Lakini alipoulizwa kuhusiana na bao la utata lililokataliwa amesema kuwa anakumbuka vizuri tukio la bao la Frank Lampard lililokataliwa na iliumiza sana ambapo alitania kuwa hakutegemea kama tukio lile linaweza kujirudia mapema kiasi hicho kuwapoza machungu waliyopata. Uingereza sasa inatarajiwa kucheza na Italia katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo Juni 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment