Sunday, June 10, 2012

HODGSON ATAMBA KUIANGAMIZA UFARANSA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema kuwa kukiongoza kikosi cha timu hiyo katika mchezo wa Kombe la Ulaya dhidi ya Ufaransa ni jambo muhimu katika maisha yake ya soka. Hogdson amesema kuwa na msisimko mkubwa kutokana na changamoto inayomkabili katika mchezo huo lakini anajua kuwa anakosolewa kama wachezaji wakishindwa kuonyesha kiwango kitakachovutia katika michuano hiyo. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa mchezo wa leo unaweza kuwa mzuri au mbaya katika maisha yake ya soka lakini yuko tayari kwa changamoto hiyo ndio maana alikubali kibarua hicho. Kikosi cha Uingereza kiliwasili nchini Ukraine Jumapili iliyopita kwa ajili ya kumalizia maandalizi yao na mchezo dhidi ya Ufaransa utakuwa ni wa kwanza kwa kocha huyo toka alipochukua mikoba hiyo kutoka kwa Fabio Capello Mei mwaka huu ambapo mchezo wao unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Donetsk Donbass Arena.

No comments:

Post a Comment