Sunday, June 10, 2012

MOROCCO YAING'ANG'ANIA IVORY COAST.

TIMU ya taifa ya Morocco imefanikiwa kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ivory Coast katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014 mchezo ambao ulichezwa jana katika Uwanja wa Grand jijini Marrakech. Ivory Coast ndiyo walioanza kuona lango la wenyeji wao katika mchezo huo baada ya bao lililofungwa na Solomon Kalou katika dakika ya nane kabla ya nahodha wa Morocco Houcine Kharja kuisawazishia timu ya bao katika dakika 39. Bao la kichwa alilofunga beki wa Manchester City Kolo Toure kufuatia mpira wa kona muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza liliiwezesha timu kuongoza karibu kipindi chote cha pili lakini Hamza Abourrouzouk alijibu mapigo kwa bao la kichwa katika dakika za majeruhi na kupelekea timu hizo kugawana pointi. Baadhi ya michezo mingine ya kutafuta tiketi ya kwenda nchini Brazil iliyochezwa jana ni pamoja na Uganda walifanikiwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Senegal, Kenya ilikubali kipigo kutoka kwa Namibia cha bao 1-0, Malawi walisimama kidete na kutoa sare ya bao bao 1-1 dhidi ya Nigeria wakati mabingwa wa Afrika Zambia walizinduka na kuifunga Ghana bao 1-0.

No comments:

Post a Comment