Sunday, June 10, 2012

LOEW AITABIRIA MAKUBWA UJERUMANI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew ametamba kuwa kuna mambo makubw yanakuja kutoka katika kikosi chake baada ya Mario Gomez kuonyesha kuwa kocha alikuwa sawa alipomuanzisha katika mchezo dhidi ya Ureno. Mshambuliaji huyo anayecheza katika klabu ya Bayern Munich bao la kichwa na kuipa ushindi wa bao 1-0 timu yake dhidi ya Ureno katika mchezo wa kundi B ikiwa muda mchache kabla ya kubadilishana na Miroslav Klose aliyetokea benchi la wachezajiwa akiba. Loew alimsifia mshambuliaji huyo kwamba ana ubora tofauti kwani alipata nafasi moja na aliitumia ipasavyo kwani katika michuano ya hiyo ya Ulaya ushindi ni kitu muhimu. Loew aliifananisha michuano hiyo kama ya mbio za magari yanayokwenda kasi ya Langalanga kwamba unaweza kupata nafasi moja tu na usipoitumia vyema basi mambo yaneweza yasiende kama ulivyotarajia. Ureno sasa itakuwa katika wakati mgumu katika kundi hilo kwani watahitajika kushinda mchezo wao unaofuata dhidi ya Denmark ambao nao waliibuka kidedea kwa kuifunga Uholanzi bao 1-0 ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment