Friday, June 22, 2012

EURO 2012 NEWS: ROBO FAINALI LEO UJERUMANI NA UGIRIKI


R
obo fainali ya Pili leo inachezwa katika Jiji la Gdansk nchini Poland ambapo miamba miwili yenye falsafa mbili tofauti ikikutana katika kuamua nani asonge mbele katika hatua ya Nusu Fainali.

Miamba hii ni Ujerumani na Ugiriki kutokana na Falsafa za kimaisha utagundua kwamba Ujerumani hujulikana kama wanaume na Wagiriki wakijigamba wao ni chimbuko la Ustaarabu wote Ulimwenguni.

Ujeumani leo haitafanya ukarimu kwa Wagiriki hao ambao hawapewi nafasi sana ya kusonga mbele kwa kuwawahisha mapema kwa mabao ili wawashushe nguvu ya kuendelea kukaba.

UJERUMANI
Timu hii ya Taifa ipo vizuri sana hasa uwepo wa Jerome Boateng ambaye amemaliza adhabu yake na leo atafanya kitu cgha kueleweka katika mechi hiyo muhimu sana kwa Ujerumani kushinda, kwani atatakiwa kuanza licha ya Lars Bender kufanya vizuri katika mechi dhidi ya Denmark.

Vijana hawa Joachim Low wana kawaida ya kukimbia na mpira kwa “speed” kutokana na wachezaji wenye spidi kali na wanaozunguka kila upande wa “pitch” hali ambayo inaweza kuwasaidia.

Licha ya kwamba Mario Gomez na Bastian Schweinsteiger kuwa wimbo kwa mashabiki lakini uwepo wa Sami Khedira ni muhimu tungeweza kusema mota ya timu kwa sasa.

Kwani Khedira na Bastian watakuwa na majukumu makubwa ya kuzunguka sana kwajili ya kuwasaidia kina Mesut Ozil, Mario Gomez na Thomas Muller.

Ukiangalia kwa makini Thomas Muller anachukua sana majukumu ya Ushambuliaji licha ya kwamba hucheza winga.

Ujerumani leo itakuwa ikikabiliw ana changamoto ya kiungo na tegemeio kuona hilo katika meci muhimu sana leo.

Ujerumani watatumia mfumo wa 4-2-3-1

UGIRIKI
Timu ya sasa ya Ugiriki inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa wachezaji wachache wenye vipaji ambapo inakutana na timu yenye mashabiki wengi wenye wachezaji wenye vipaji hivyo itawawia vigumu kuitandika Ujerumani.

Kocha Santos anakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa Skipper Giorgos Karagounis katika mechi ya leo kwani uwepo wake huweza sababisha kitu pia mlinzi wake Jose Holebas ambao wanakabiliwa na adhabu.

Pia hawatakuwa na mlinda mlango Kostas Chalkias katika mechi hii kutokana na majeruhi aliyoyapata katika mechi dhidi ya Poland.

Tegemea kuona Ugiriki ikilinda sana lango lake hii leo kwa kuupiga chini mfumo wa 4-2-3-1 na kuutumia 4-5-1 kukabiliana na Ujerumani.

Key Match Facts
·         Tangu mwaka 2004 Ujerumani imekuwa ikifika Robo Fainali au zaidi ya hapo katika mashindano makubwa.
·         Ugiriki katika michuano ya EURO wamefika mara moja mwaka 2004 na ndio mwaka waliochukua Kombe hilo.
·         Katika Historia inaonyesha Ujerumani haijawahi kupoteza kwa Ugiriki. Amemtandika mara 5 na kutoa sare mara 3 katika mara 8 walizokutana.
·         Ugiriki ilifuzu michuano ya Euro 2012 kwa kufunga mabao 14 katika mechi 10 walizocheza, wakati Ujerumani walifuzu kwa kutupia wavuni mabao 34 katuika mechi hizo.
PLAYERS TO WATCH
Mesut Ozil (The German Maestro)
LINE UPS

Euro Record
Greece :
Winners: 2004
Germany:
Winners: 1972, 1980, 1996
Runners up: 1976, 1992, 2008

 

No comments:

Post a Comment