Tuesday, June 26, 2012

DESCHAMPS AIKACHA MARSEILLE.

KOCHA wa klabu ya Olympique de Marseille ya Ufaransa, Didier Deschamps ameamua kujiuzulu kuinoa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Ligue 1. Marseille inatarajiwa kuanza mazoezi Julai 1 mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi lakini itabidi wafanye hivyo bila ya kuwepo kwa Deschamps ambaye pia amewahi kuzinoa klabu za Monaco na Juventus ya nchini Italia. Kocha amesema kuwa klabu hiyo haionyeshi nia nia ya kupata mafanikio baada ya kumaliza katika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligue 1 msimu uliopita pamoja na kushindwa kuelewana ana Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Jose Anigo katika baadhi ya mambo ya kiufundi ya klabu hiyo. Marseille bado haijakubali barua ya kujiuzulu ya Deschamps lakini inaonekana wanasubiri muda kidogo iliwatangaze rasmi kuondoka kwa kocha huyo ambaye amewahi pia kuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Deschamps mwenye umri wa miaka 43 anahusishwa na tetesi za kuchukua mikoba ya kocha Laurent Blanc katika kikosi cha Ufaransa baada ya kuondolewa kwa timu hiyo kwenye michuano hiyo na pia amekuwa akihusishwa na tetesi za kuziba pengo la aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspurs Harry Redknapp.

No comments:

Post a Comment