Tuesday, June 26, 2012

NASRI HATARINI KUFUNGIWA MIAKA MIWILI.

KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa, Samir Nasri huenda akafungiwa kucheza michezo ya kimataifa kwa miaka miwili baada ya kumshambulia mwandishi wa habari katika michuano ya Ulaya mwaka huu. Kiungo huyo alikwaruzana na mwandishi wa Ufaransa baada ya timu hiyo kung’olewa katika robo fainali ya michuano ya Ulaya baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Hispania. Nasri ambaye aliingia katika mchezo huo kama mchezaji wa akiba alimjibu mwandishi huyo kwa lugha chafu baada ya kuulizwa swali kuhusiana na mchezo huo mara baada ya kumalizika. Hiyo inakuwa ni mara ya pili kwa mchezaji huyo kuingia katika mzozano na mwandishi huyo ambapo mara kwanza alishangilia bao akimwambia mwandishi huyo kufunga mdogo wake wakati alipofunga bao ya kusawazisha dhidi ya Uingereza katika mchezo wa ufunguzi wa kundi D dhidi ya Uingereza. Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa-FFF, Noel le Graet amesema kuwa tukio alilofanya mchezaji huyo halivumiliki na kumuonya Nasri kuwa anapaswa kuzuia hasira zake katika siku mbeleni.

No comments:

Post a Comment