Tuesday, June 26, 2012

ARSENAL YAKAMILISHA USAJILI WA GIROUD.

Klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza imefanikiwa kumnyakuwa mshambuliaji Olivier Giroud kutoka klabu ya Mintepellier kwa ada ya paundi milioni 12. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 alikamilisha vipimo vya afya na kufuzu jana jioni na kuwa mchezaji rasmi wa klabu hiyo ambapo ataungana na nyota wengine kama Lucas Podolski ambaye nae amesaini msimu huu akitokea Ujerumani na Robin van Persie. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa amefurahishwa na ujio wa mchezaji huyo kwani anaweza kuisaidia timu hiyo katika kampeni zake za kuwinda vikombe ambavyo wamevikosa kwa takribani miaka saba sasa. Giroud amefunga mabao 21 katika Ligi Kuu nchini Ufaransa au Ligue 1 akiwa na timu ya Montpellier msimu uliopita na pia amecheza katika michezo minne ya Ufaransa akitokea benchi la wachezaji wa akiba katika michuano ya Ulaya inayoendelea huko Poland na Ukraine.

No comments:

Post a Comment