Saturday, June 9, 2012

DEMBA BA KUIKOSA UGANDA.



WACHEZAJI watano wa timu ya taifa ya Senegal wanatarajiwa kukosa mchezo wa leo wa kuvuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya timu ya taifa ya Uganda kutokana na kuwa majeruhi. Wachezaji ambao wanatarajia kukosa mchezo huo ni mshambuliaji nyota wa timu hiyo Demba Ba, Moussa Sow, Issiar Dia, Kader Mangane na Souleymane Diawara. Pamoja na kuwakosa wachezajo wote hao watano, nahodha wa kikosi hicho Papiss Demba Cisse na kocha wa timu hiyo Joseph Koto wana imani ya kufanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya Uganda. Koto amesema kuwa kutokana na uwepo wa Papiss Cisse, Souleymane Camara na Dame ndoye ambao walikosa baadhi ya michezo huko nyuma ana imani kikosi hicho kitapata matokeo mazuri katika mchezo huo. Mchezaji mwingine wa kikosi hicho Mamadou Niang ambaye ameamua kupumzika soka la kimataifa hatakuwemo katika kikosi cha timu hiyo.

No comments:

Post a Comment