Saturday, June 9, 2012

LOEW AMTEGEMEA OZIL KUITUNGUA URENO.KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amesema kuwa anamtegemea kiungo wake Mesut Ozil kufunga mabao zaidi kwa timu hiyo wakati watakapocheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ureno baadae leo. Ozil ambaye ameifungia Ujerumani mabao nane katika michezo 33 aliyocheza ni mmoja ya wachezaji bora zaidi katika kikosi hicho na alikuwa na msimu wenye mafanikio wakati akiwa katika klabu yake ya Real Madrid. Loew ambaye amesema kuwa kiwango cha ozil kimepanda toka atue Madrid mwaka 2010 kwani sasa ni mchezaji aliyekomaa na anayejiamini zaidi, ameweka wazi kuwa lazima mchezaji huyo mwenye miaka 23 ang’ae katika michuano hiyo. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa tofauti na wachezaji wengine katika kikosi chake Ozil ni aina ya mchezaji aliezoea michuano mikubwa akiwa amecheza michuano ya Kombe la Dunia 2010 hivyo ni matumaini yake atafanya vizuri katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment