Sunday, June 17, 2012

SHEVCHENKO HATIHATI KUIVAA UINGEREZA.


 

MSHAMBULIAJI nyota na nahodha wa timu ya taifa ya Ukraine, Andriy Shevchenko ameshindwa kuhudhuria mazoezi ya timu yake jana hivyo kuzusha mjadala kama mchezaji huyo atajumuishwa katika kikosi kitakachoivaa Uingereza katika mchezo wa kundi D wa michuano ya Ulaya. Shevchenko mwenye umri wa miaka 35 alikuwa amekaa katika benchi wakati wenzake wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Donetsk ambapo msemaji wa timu hiyo amesema kuwa mchezaji huyo amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mguu. Mchezaji huyo alifunga mabao mawili na kuiwezesha timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sweden na kama asipocheza mchezo dhidi ya Uingereza utakaopigwa kesho basi kocha wa timu hiyo Oleh Blokhin anatarajiwa kumtumia Marko Devic kuziba pengo lake. Ukraine mpaka sasa wana alama tatu katika kundi D huku Uingereza na Ufaransa zote zikiwa na alama nne kila moja wakati Sweden wenyewe wameshatolewa baada ya kukosa alama zozote katika michezo yao miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment