Tuesday, June 26, 2012

BOSI URUSI ABWAGA MANYANGA.

Sergei Fursenko.
OFISA mkuu wa Chama cha Soka cha Urusi-RFU, Sergei Fursenko amejiuzulu wadhfa wake huo kufuatia matokeo mabaya iliyopata nchi hiyo katika michuano ya Ulaya inayofanyika Poland na Ukraine. Fursenko ambaye pia ni mjumbe katika bodi ya Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA alijiuzulu baada ya kufanya mazungumzo na Rais wan chi hiyo Vladimir Putin. Fursenko amekuwa akiandamwa na mashabiki wa soka wan chi hiyo kufuatiwa kiwango kisicho cha kuridhisha kilichooneshwa na timu hiyo katika michuano hiyo na kupelekea kuenguliwa katika hatua mwanzo. Ofisa huyo ambaye ana umri wa miaka 58 aliteuliwa kuiongoza RFU Februari mwaka 2010 baada ya kufanya kazi kama rais wa klabu ya Zenit St PetesBurg ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Italia kwa miaka minne. Yeye ndio amekuwa kichocheo kikubwa cha kumwajiri Dick Advocaat kuwa kocha wa nchi hiyo mwaka 2010 baada ya kuamua kutomwongeza mkataba Guss Hiddink ambaye alikiongoza kikosi cha nchi hiyo kufika hatua ya nusu fainali katika michuano ya Ulaya mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment