Tuesday, June 26, 2012

UEFA YAIPIGA FAINI DFB.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limekipiga faini ya euro 25,000 Chama cha Soka cha Ujerumani-DFB kutokana na tabia isiyofaa iliyoonyeshwa na mashabiki wa timu ya taifa ya nchi hiyo wakati wa mchezo wa kundi B ambapo Ujerumani ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Denmark Juni 17 mwaka huu. Mashabiki wa nchi hiyo walikuwa wakiwasha mafataki na kuonyesha mabango ambayo ambayo hayaruhusiwi katika michuano hiyo ambayo yanachochea ubaguzi katika mchezo wa soka. Faini hiyo inakuwa sio ya kwanza kwa DFB ambapo tayari walishatozwa faini ya euro 10,000 wakati mashabiki wa Ujerumani waliporusha karatasi ambao walikuwa wameikunja mfano wa ndizi kwa wachezaji wa Ureno katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa June 9 jijini Lviv. Ujerumani ambao wameshinda michezo yao yote minne waliyocheza na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na Italia katika Uwanja wa Taifa jijini Warsaw, Poland, wanaweza kukata rufani kupinga adhabu hiyo lakini inatakiwa iwasilishwe ndani ya masaa 24.

No comments:

Post a Comment