Friday, June 15, 2012

BENDTNER KUJADILIWA UEFA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Denmark, Nicklas Bendtner anaweza kukabiliwa na adhabu kutoka Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA baada ya kuonyesha nembo ya kampuni ya bahati nasibu iliyokuwa katika nguo yake ya ndani wakati akishangilia bao wakati wa michuano ya Ulaya. Bendtner alinyanyua fulana yake kuonesha nembo hiyo baada ya kufunga bao la pili katika kundi B uliochezwa Jumatano ambapo Denmark walifungwa mabao 3-2. Taarifa iliyotumwa na UEFA imesema kuwa shirikisho hilo litamfungulia mashtaka mshambuliaji huyo kwa kukiuka maadili wakati wa mchezo huo uliochezwa jijini Lviv na shitaka lake litasikilizwa Jumatatu. UEFA pamoja na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA limeweka sheria kali ya kuzuia fulana au nguo yoyote yenye nembo ya kampuni ambao sio wadhamini rasmi kutumiwa na wachezaji ili kulinda makampuni ya matangazo ambayo yanalipa mamilioni kwa ajili udhamini wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment