Tuesday, June 19, 2012

BENDTNER AFUNGIWA MECHI MOJA.


 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Denmark, Nicklas Bendtner amefungiwa mchezo mmoja wa mashindano na kutozwa faini ya euro 100,000 baada ya kuonyesha nguo yake ya ndani ambayo ilikuwa na tangazo wakati wa mchezo dhidi ya Ureno. Bendtner ambaye ana umri wa miaka 24 alionyesha nembo ya kampuni ya bahati nasibu katika nguo yake ya ndani wakati akishangilia bao la pili wakati wa mchezo dhidi ya Ureno ambao walifungwa mabao 3-2. Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA limemuadhibu mchezaji huyo anayecheza klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa utovu wa nidhamu ambapo amepewa siku tatu za kukata rufani juu ya adhabu ya aliyopewa. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Bendtner ambaye msimu uliopita alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sunderland amesema kuwa hakujua kama alichokifanya kilikuwa ni kosa na anashukuru kwakuwa sasa analitambua hilo.

No comments:

Post a Comment