Tuesday, June 19, 2012

ATLETICO MADRID YAMNYAKUWA DIAZ.

Daniel Diaz.


KLABU ya Atletico Madrid imefikia makubaliano ya kumsainisha beki wa wa kimataifa wa Argentina, Daniel Diaz kutoka klabu ya Getafe kwa mkataba wa miaka miwili. Beki huyo wa wa kati wa zamani wa klabu ya Boca Juniors ambaye ana umri wa miaka 33 ameitumikia klabu ya Getafe kwa muda wa miaka mitano. Mkurugenzi wa Michezo wa Atletico, Luiz Perez Caminero amesema katika taarifa yake kuwa mchezaji ana kiwango na uzoefu wa kutosha ambao atasaidia kuwakuza wachezaji vijana wa klabu hiyo. Diaz anakuwa mchezaji watatu kuongeza nguvu katika klabu hiyo baada pia kuwasajili mshambuliaji wa kimatifa wa Uruguay Cristian Rodriguez na kiungo wa Uturuki Emre Belozoglu.

No comments:

Post a Comment