Tuesday, June 19, 2012

MMOJA AFARIKI KATIKA SHAMBULIO LA RISASI.


 

POLISI wanamtafuta mtuhumiwa ambaye alifanya shambulio la risasi nje ya duka moja katika jiji la Toronto nchini Canada ambapo kulikuwa na mamia ya mashabiki wa soka waliokuwa wakitizama mechi za Kombe la Ulaya. Katika tukio hilo polisi wanasema mtu mmoja alikufa na mwingine kujeruhiwa na kukimbizwa hospitalini lakini hakuwa na majeraha ya kutisha. Msemaji wa polisi wa eneo hilo Wendy Drummond amesema kuwa tukio hilo limetokea eneo ambalo kuna wakazi wengi raia wa Italia ambao walikusanyika kuitazama timu yao ya taifa ikicheza na Ireland. Matukio ya risasi limekuwa kama suala la kawaida katika eneo hilo ambapo mwezi uliopita watu wawili walikufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tukio kama hilo na polisi wanahisi kuwa watuhumiwa wanaofanya matukio hayo wanatoka katika kundi moja.

No comments:

Post a Comment